Friday, March 16, 2012

MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM ARUMERU ULIVYOKUWA MACHI 14!

Meneja kampeni za CCM,uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Mwigulu Nchemba (kulia) akimnadi mgombea wa CCM jimbo hilo, Sioi Sumari katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, 14/4/12 katika kijiji cha Shambarai, Kata ya Mbuguni.
Wananchi wa kijiji cha Shambarai, Kata ya Mbuguni, wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimboni humo leo.
Mgombea ubunbge wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akiwaalimia wakati wa kijiji cha Shambarai Kata ya Mbuguni kabla ya mkutano wa kampeni za CCM leo.
Pamela Sioi akimuombea kura mumewe, mgombea ubunge wa CCM, jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari kwenye kampeni zilizofanyika kijiji cha Shambarai kata ya Mbuguni jimboni humo leo.
Mama Sioi(wapili kulia) akihiriki kuselebuka muziki wa hamasa za Chama, uliporomoshwa katika kijiji cha Msitu wa Mbogo kata ya Mbuguni kabla ya kuanza kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimboni humo leo.
Sioi Sumari akiwaaga wapigakura wake baada ya kumaliza mkutano katika kijiji cha Msitu wa Mbogo.
"Tupo na ninyi" wanafunzi wa shule ya msingi Msitu wa Mbogo wakisema huku wakionyesha dole gumba msafa wa mgombea ubunge wa CCM Sioi Sumari ulipowasili kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja uliopo jirani na shule hiyo katika kata ya Mbuguni.

No comments:

Post a Comment