Friday, January 13, 2012

RASHID MATUMLA VS MANENO OSWARD KUPAMBANA TENA FEBRUARI 25 UKUMBI WA PTA SABASABA DAR

 MAANDALIZI ya pambano lisilo la ubingwa kati ya mabondia Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ lililopangwa kuwa Februar 25 mwaka huu yanaenda vizuri.Promota wa mpambano huo Issa Malanga, alisema pambano hilo limeandaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao, ambao pambano la mwisho walitoka sare ya point 99.99


Hata hivyo Oswald aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki. Mabondia hao wamewahi kupambana mara nne, Oswald akishinda mara moja na Matumla mara mbili na kutoka sare mara moja.Alisema pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati, litafanyika kwenye ukumbi wa PTA sabasaba Dar es salaam

Mpambano huo wa kumaliza ubishi baada ya kila mmoja wao kudai alishinda katika mpambano wao wa mwisho. Aidha aliwataja wakali watakaosindikiza mpambano huo ni Shomali Mirundi na Mikidadi Abdallah 'Tatson', na Iddy Mkenye atapambana na Shabani Mtengela ' Zunga Boy', Abdallah Mohamedi na Saleh Mkalekwa mbali na hayo mpambano mwingine ni Ramadhani Mashudu na Hassani Kiwale 'Moro Best


Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.


“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

No comments:

Post a Comment