Sunday, January 29, 2012

KCB ILIPOZISAIDIA HOSPITALI ZA BUGURUNI NA CCBRT MSAADA WA VIFAA TIBA!

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania DK Edmund Mndolwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Vitanda vya wajawazito kwa hospitali ya Buguruni vya Zaidi ya shilingi milioni Nane jijini Dar es SalaamMwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, DK Edmund Mndolwa (kushoto) akimkabidhi moja ya kitanda cha kujifungulia wajawazito, Daktari Mfawidhi wa  hospitali ya Buguruni, Hawa  Lesso  wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali  hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine katikati ni Mkurugenzi wa KCB, Moezz Mir  na Mwenyekiti wa Hospitali hiyo Fatma Faki.Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Edmund Mndolwa akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 13 Mkurugenzi msaidizi wa hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla  kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vya hospitali  wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mwingine ni  Mkurugenzi Mtendaji wa wa KCB, Moezz Mir.Mkurugenzi wa Mtendaji KCB Tanzania, Moezz Mir akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 13 Mkurugenzi Msaidizi wa hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla  kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vya hospitali  wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, DK Edmund Mndolwa.

No comments:

Post a Comment