Saturday, August 13, 2011
WAREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA WATEMBELEA HIFADHI YA MIKUMI!
Warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika bwawa la Viboko lililopo katika Hifadhi ya Wanyama pori Mikumi mkoani Morogoro jana wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo kujionea wanyama aina mbalimbali ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii nchini kuhamasisha utalii wa ndani. (Picha na Mpigapicha wetu).
KCB TANZANIA YAMUAGA JORAM KIARIE ANAYERUDI KCB MAKAO MAKUU!
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Edmund Mndolwa (kushoto) akimkabidhi zawadi ya ngao Mkurugezi wa Benki hiyo anayemaliza muda wake, Joram Kiarie baada ya kuitumikia wa kipindi cha miaka 6 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCB Kenya, Peter Muthoka (kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCB Tanzania, Edmund Mndolwa na Mkurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Joram Kiarie wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya kuwaaga baadhi ya Wakurugenzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Edmund Mndolwa akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga baadhi ya Wakurugenzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Edmund Mndolwa akimkabidhi zawadi ya mchoro wa Gofu Zanzibar kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCB Kenya, Peter Muthoka wakati wa hafla ya kuwaaga baadhi ya Wakurugenzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye akiwa na moja ya zawadi ambayo alikabidhiwa mmoja ya Wakurugenzi wa benki hiyo wakati wa hafla ya kuwaaga baadhi ya wakurugenzi wa benki jijini Dar es Salaam.
Wenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB na Baadhi ya Wakurugenzi wa benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kuwaaga baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.

CHODAWU YAVUNJA KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA!
Anna Titus na Esther Muze
Maelezo,Dar es Salaam
Baraza kuu maaluum la CHODAWU limevunja kamati ya utendaji ya Taifa iliyokuwepo na kutengua uteuzi wa aliyekuwa anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu Bwana Kiwanga Towegale.
Taarifa iliyotumwa kwa Idara ya Habari (MAELEZO) iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza Kuu maalum Bwana Paul Msilu imesema licha ya kutengua nafasi ya Katibu Mkuu CHODAWU baraza hilo limeondoa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu aliyokuwa nayo Bwana Francis Maembe.
Aidha Baraza hilo limechagua Kamati mpya ya utendaji ya Taifa itakayosimamia shughuli za uendeshaji kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu ambayo itaongozwa na Bwana Said Wamba.Taarifa hiyo imefafanua kuwa,Bwana Said Wamba ataiongoza Kamati mpya ya utendaji ya Taifa katika kipindi cha mpito cha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mapema mwanzoni mwa mwezi Septemba 2011.
Pia Baraza Kuu limeomba wanachama na wadau wote kutoa ushirikiano kwa Kamati hiyo mpya katika kutekeleza jukumu la kuratibu shughuli zote za uchaguzi. Maamuzi ya Baraza hilo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mbezi Garden Jijini Dar es Salaam tarehe 3,Agosti 2008.
WREMBO WA VODACOM MISS TANZANIA WAINGIA KATIKA JUMBA LA VODACOM!
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwakaribisha mshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, Mariaclara Mathayo katika Jumba la Vodacom ambalo litatumika katika kipindi chote cha warembo wakiwa kambini. Katikati ni Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Vodacom Miss Tanzania, Hashim Lundenga. Warembo hao wameingia katika Jumba hilo Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkaribisha mshiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, Cynthia Kimasha katika Jumba la Vodacom ambalo litatumika katika kipindi chote cha warembo wakiwa kambini. Katikati ni Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Vodacom Miss Tanzania, Hashim Lundenga. Warembo hao wameingia katika Jumba hilo rasmi Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba (katikati) akiwafundisha namna ya kufungua shampeni warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, muda mfupi baada ya warembo hao 30 kuingia katika Jumba la Vodacom lililopo jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba (katikati) akigonganisha chupa za shampeini na warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, muda mfupi baada ya warembo hao 30 kuingia katika Jumba la Vodacom lililopo jijini Dar es Salaam jana.
Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakigonganisha glasi zao za shampeni muda mfupi baada ya warembo hao 30 kuingia katika Jumba la Vodacom lililopo jijini Dar es Salaam jana. Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakicheza kwaito wakati wa tafrija maalum ya kuwakaribisha katika Jumba la Vodacom lililopo jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya warembo 30 waliingia katika jumba hilo kwa kambi yao.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akizungumza jambo na warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, baada ya kuingia katika Jumba la Vodacom jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Mpigapicha wetu).
Subscribe to:
Posts (Atom)