Chama cha Wananchi CUF kimesema malumbano ya kupinga mchakato wa utiaji saini muswada wa Katiba mpya yanayofanywa na baadhi ya vyama vya siasa hauna maana kwa sasa kwani Watanzania wanahitaji kupata katiba mpya kabla ya kufikia mwaka 2015.
Kuhusiana na suala la viongozi wa CUF kukutana na Rais JAKAYA KIKWETE, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi JULIUS MTATIRO amesema walionana na rais ili kushinikiza mapendekezo yote yaliyopo kwenye muswada wa uundwaji wa katiba mpya yafanyiwe kazi.
No comments:
Post a Comment