Monday, December 19, 2011

CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TIBA IMTU CHATAMBULIWA NA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI!

Chuo Kikuu cha sayansi na Tiba IMTU kimeweza kupata utambuzi na shirika la afya duniani, utakaowawezesha madaktari wanaohitimu katika chuo hicho kupata kazi za udaktari kote ulimwenguni.

Mkuu wa chuo cha IMTU Prof JOSEPH SHIJA, amesema chuo hicho kimejipanga kuzalisha wataalamu mahiri kwenye sekta ya afya, na kwamba chuo hicho kinatarajia kutoa wahitimu zaidi ya 190 wa fani mbali mbali za udaktari na uuguzi, katika mahafali yake ya tano yatakayofanyika jumatano wiki hii.


Katika hatua nyingine mkuu huyo amesema bodi ya wadhamini wa chuo hicho, wamekubali ombi la serikali la kuwataka wanafunzi wote wakitanzania shuleni hapo, kulipa ada zao kwa kutumia shillingi ya Tanzania badala ya Dola ya marekani.

No comments:

Post a Comment