Moja ya nyumba zinazomilikiwa na NHC
Msajili wa Hazina ameagizwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma kuwasilisha kwenye kamati hiyo orodha ya mashirika ya Umma ambayo yamekuwa hayapeleki Serikalini asilimia kumi ya faida wanayopata na hivyo kuinyima mapato Serikali.
Hatua hiyo imekuja wakati kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ilipokutana na Uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC na kulipongeza shirika hilo kwa hatua yake ya kukusanya madeni sugu bila kubagua aina ya wadaiwa.
Akizungumza kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo na mbunge wa Ludewa Bwana DEO PHILIKUNJOMBE ameitaka NHC kuboresha mfumo wa kuhifadhia kumbukumbu, kuweka utaratibu wa bima kwa mali zake na kuwaingiza watumishi wake kwenye utaratibu wa Bima ya Afya.
Naye mwenyekiti wa Bodi ya NHC Bwana KESOGUKEWELE MSITA amesema mafanikio katika shirika hilo yametokana na uongozi bora huku akitambua mchango wa vijana.
No comments:
Post a Comment