Wednesday, October 5, 2011
MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU YA WIZARA YA AFYA YALIVYOFUNGWA!
Mshehereshaji katika sherehe za kufungwa kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru na Utoaji huduma za Afya Tanzania MC Peter Mavunde zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin.
Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin akizungumza wakati wa kufungwa kwa maadhimisho hayo ambapo ameipongeza Tanzania kwa Mafanikio iliyofikia katika utoaji huduma za Afya katika Kipindi cha Miaka 50 iliyopita haswa katika kupunguza vifo vya watoto wadogo ambapo Tanzania kwa sasa imefanikiwa kupunguza vifo 110.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Dkt. Lucy Nkya akitoa hotuba ya kufunga maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru na Utoaji Huduma za Afya Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia mafanikio yaliyofikiwa katika kutoa huduma ambazo hazikuwa zikipatikana hapa nchini kama vile Tiba ya Mfupa na Viungo, Upasuaji wa Moyo, Saratani na Tiba ya Magonjwa ya Figo pamoja na kusafisha Damu.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara na Serikali na wadau wa Sekta ya Afya nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment