David Kafulila (Katikati)
Tanzania inaenda kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wakati uchumi wake ukikabiliwa na tofauti kubwa ya kimapato baina ya kundi la Watanzania makabwela na lile la walio nacho ambao wamekuwa wakiishi kwa kukata tamaa kutokana na matabaka hayo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara kuelekea miaka 50 ya Uhuru kwenye viwanja vya Temeke Jijini DSM Mbunge wa Kigoma Kusini DAVID KAFULILA amesema uchumi wa kundi la walionacho ambao ni Mawaziri, Wabunge, Maktibu Wakuu na Wafanyabiashara wakubwa unakuwa wakati ule wa makabwela ukiporomoka zaidi.
Kutokana na hilo Mheshimiwa KAFULILA ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa NCCR – Mageuzi ametoa wito kwa serikali kufikiria upya uamuzi wa kujiunga kwenye soko la pamoja la Afrika Mashariki ili kuepuka wananchi kuishia kuwa vibarua.
No comments:
Post a Comment