Serikali imesema kila mzazi anao wajibu wa kumtunza mtoto wake badala ya kumtumia kama kitega uchumi kwa njia ya kuomba omba ovyo mitaani.
Akijibu swali Bungeni mjini Dodoma Naibu waziri wa afya na ustawi wa Jamii Dakta LUCY NKYA amekemea hatua ya baadhi ya wazazi nchini kuacha kuwapeleka watoto wao Shuleni na badala yake wamekuwa wakiwatumia mitaani kuomba omba kwa lengo la kujipatia fedha za kujikimu kuliko kujishughulisha.
Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto namba 2 ya mwaka 2009, ni kosa kwa mzazi ama mlezi kumtumia mtoto kama ombaomba kwa sababu kufanya hivyo kunamkosesha mtoto haki zake za msingi za kupata elimu ambayo ndio ufunguo wa maisha yake.
No comments:
Post a Comment