Mdau wa michezo Amir Mohamedi 'Msauzi' akimkabidhi maji kwa niaba ya mdau Prince Muddy Kalla wa Ilala kwa Kocha wa Mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' katoni 15 za maji kwa ajili ya mashindano ya kuhamasisha mchezo wa ngumi itakayofanyika jumapili ya Julai 17.
Mdau wa michezo Amir Mohamedi 'Msauzi' akimkabidhi maji kwa niaba ya mdau Prince Muddy Kalla wa Ilala kwa Kocha wa Mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' katoni 15 za maji kwa ajili ya mashindano ya kuhamasisha mchezo wa ngumi itakayofanyika jumapili ya julai 17.
Mdau wa michezo Amir Mohamedi 'Msauzi' akimkabidhi maji kwa niaba ya mdau Prince Muddy Kalla wa Ilala kwa Kocha wa Mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' katoni 15 za maji kwa ajili ya mashindano ya kuhamasisha mchezo wa ngumi itakayofanyika jumapili ya julai 17.
Na Mwandishi Wetu.
MCHAKATO wa Kuendeleza mchezo wa ngumi za Ridhaa Katika Mkoa wa Kimichezo wa ILALA, natarajiwa kuingia katika hatua nyingine Julai 17 kati ya klabu za ngumi ya Amana, Matimbwa, Ashanti, Bigrayt na klabu nyingine
Mapambano hayo ya raundi nne, yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi uliopo bungoni Wilaya ya ILala ambapo mabondia wanne kutoka katika kila klabu, watachapana makonde.
Mabondia wa Amana watakaopanda siku hiyo ni IBrahimu Class Kg.64, Khalfani Othumani Kg 57, Kassimu Sambo Kg 54, na Saidi Ally Kg 48. Klabu ya Matimbwa itawakilishwa na MOhamedi Matimbwa Kg 64, MOhamedi Muhani Kg 57, Edson Joviki Kg 54 na MOhamedi Kumbilambali Kg 48 na Klabu ya Ashanti ni Uwesu Manyota,Ramadhani Kimangale,Mark Edson.
Akizungumza Dar es Salaam leo Mratibu wa mapambano hayo ambae pia ni kocha wa mchezo wa ngumi akishirikiana na Kinyogoli Foundition, Rajabu Mhamila Super D, Alisema mpango huo utaendelea mpaka wahakikishe wamefanikiwa kuibua vibaji na kuviendeleza.
Alisema tangu waanze mpango wa kuandaa mapambano mkohani humo wamefanikiwa kurudisha hamasa ya mchezo huo mkoani humo na kuwataka wadau mbalimbali kutoa sapoti kwa mchezo huo ili upate kuendelea ambapo Super D alitoa mfano wa vitu wanavyoviitaji ikiwemo posho za nauli kwa wachezaji vifaa vya kuwatia moyo na zawadi mbalimbali kwa mabondia
Super D aliwashukulu wadau waliojitolea katoni 15 za maji kwa ajili ya kuendesha mashindano hayo yatakayofanyika jumapili ya Julai 17 aliwataja waliosaidia kuwa Mohamed Sadiq 'Muddy Kala' na Mwanamama Halima Kaubanika aliyejitolea maji kwa wachezaji wote watakaocheza kwa siku hiyo.
No comments:
Post a Comment