Wednesday, June 8, 2011

SERIKALI YAANZA KUUZA MAHINDI KUTOKA KWENYE HIFADHI ILI KUPUNGUZA BEI YA UNGA KWENYE MIJI MIKUBWA!

                           Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. JUMANNE MAGEMBE
Serikali imesema imeanza kuuza mahindi kutoka hifadhi ya taifa ya chakula ili kujaribu kuteremsha bei ya chakula hasa mahindi nchini kwa ajili ya mikoa ambayo bei ya unga iko juu hususani katika miji mikubwa.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. JUMANNE MAGEMBE amesema Bungeni mjini Dodoma kwamba kwa bidhaa hiyo imekuwa ikinunuliwa kwa wingi na wafanyabaishara kutoka nchi jirani na wanashindwa kuzuia hali hiyo kwa kuwa ni fursa kwa wakulima kunufaika na nguvu kazi zao.
Mbunge wa Viti Maalumu, Betty Machangu (CCM) katika swali lake la msingi aliiuliza serikali ina mpango gani wa kuongeza bei ya mahindi ili wakulima wasishawishike kuuza mazao yao nje ya nchi hali inayochangia uhaba wa chakula nchini.

No comments:

Post a Comment