Naibu Waziri wa Fedha GREGORY TEU (Kulia)
Mlango wa Bandari jijini Dar es Salaam.
MUSSA AZAN ZUNGU akiwa na Waziri Mkuu MIZENGO PINDASerikali kupitia Wizara ya Fedha imesema ili kuboresha utoaji wa huduma za uingizaji na usafirishaji mizigo kupitia bandari nchini imepanga kuboresha kiwango cha matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwa ni pamoja na kuongeza muda wa kutoa huduma hiyo kufikia saa ishirini na nne kwa siku.
Akijibu swali la Mbunge wa Ilala MUSSA AZAN ZUNGU, Naibu Waziri wa Fedha GREGORY TEU amesema mpango huo umefikiwa baada ya serikali kubaini kwamba kuongeza muda wa utoaji huduma bila kuboresha matumizi ya vifaa vinavyotumia teknolojia ya kisasa msongamano wa mizigo bandarini na mipakani hautapungua.
MUSSA ZUNGU katika swali lake la nyongeza aliuliza serikali ina mkakati upi wa kuongeza kiwango cha utoaji huduma kwenye bandari na mipaka ya nchi jirani ili kuepuka kukimbiwa na wateja kutokana na ghamara kubwa za kupitisha mizigo katika maeneo hayo kuliko kwenye viwanja vya ndege.
No comments:
Post a Comment