Monday, June 27, 2011

KAWE UKWAMANI KUOMBA MSAADA ILI IZOLEWE TAKATAKA!

Serikali ya Mtaa wa Ukwamani, Kawe Jijini Dar es salaam, imepanga kuomba msaada kwa taasisi mbalimbali nchini zinazojihusisha na uzoaji taka ili ziwasaidie kuzoa takataka zilizorundikana kwenye eneo hilo.



Akizungumza na kituo hiki, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Ukwamani, ABDUL SALUM amesema mtaa huo umeamua kuomba msaada huo kutoka kwa wahisani mbalimbali kutokana na Manispaa kushindwa kukabiliana na tatizo la taka hizo.Aidha amewataka wananchi wa eneo hilo kuachana na tabia ya kutupa taka eneo hilo kufuatia kuwepo kwa uwezekano wa kukabiliwa na magonjwa ya mlipuko.

No comments:

Post a Comment