Tuesday, June 21, 2011

JAJI BOMANI AMWOMBA RAIS KIKWETE AACHE MCHAKATO HURU WA UUNDWAJI WA KATIBA!

Rais JAKAYA KIKWETE ameombwa kuchagua jopo la wawakilishi wenye fikra mbalimbali ili kupendekeza mchakato wa Katiba mpya ambao watakusanya maoni huru kutoka kwa wananchi.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano lililoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania MCT Jaji Mstaafu MARK BOMANI amesema licha ya jopo hilo kuwa na kazi ya kupendekeza aina ya hadidu za rejea zinazofaa pia lipewe nafasi ya kuwashirikisha wananchi katika uundwaji wa katiba hiyo mpya.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa MCT KAJUBI MKAJANGA amesema lengo la mjadala huo uliohusisha Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini na watunga sera ni kukumbusha mchango wa wanahabari katika kufikia mchakato wa upatikanaji wa katika mpya.

No comments:

Post a Comment