Muungano wa Asasi za Ki-raia zipatazo 50 zinazotetea usawa wa Jinsia,Haki za Binadamu pamoja na Ukombozi wa wanawake Kimapinduzi (Femact) umepinga hatua ya Serikali kuruhusu wasichana 40 kwenda nchini Swaziland kujifunza kucheza Ngoma ya Asili nchini ambayo imekuwa ikidhalilisha utu wa mwanamke.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa jijini DSM na muungano na kusainiwa na Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Bi USSU MALLYA imesema kwamba Ngoma hiyo ambayo ni maarufu nchini Swaziland imekuwa na maudhui ya kumdhalilisha mwanamke ikiwa ni kinyume na lengo la uanzishwaji wake.
Aidha Muungano huo umemtaka Rais JAKAYA KIKWETE kuusitisha mpango huo,na kuongeza kuwa Ngoma hiyo ya udhalilishaji imekuwa ikipingwa vikali na wanaharaki wa masuala ya kijinsia nchini Swaziland.
No comments:
Post a Comment