Wednesday, June 29, 2011

CCM YAMWAGIZA WAZIRI KUMCHUKULIA HATUA MHANDISI WA MAJI TANDAHIMBA!

NA BASHIR NKOROMO, TANDAHIMBA


CHAMA cha Mapinduzi(CCM) kimemtaka Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya kumchukulia hatua Mhandisi Mkuu wa Maji wilayani Tandahimba mkaoni Mtwara kwa kudaiwa kuwakoroga wananchi katika kusimamia huduma za maji katika wilaya hiyo na Newala. Mkurugenzi huyo ambaye ni msimamizi wa mradi wa maji wa Makondeko, ambao chanzo chake cha maji kipo Newala, anadaiwa kujihusisha na biashara ya kuuza maji na hivyo kula njama yasipatikane katika maeneo mengi katika wilaya hizo ili aweze kufanya biashara yake vizuri.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wilayani hapa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye alisema kuhusu kero hiyo, maelekezo ya mkurugenzi huyo kuchukuliwa hatua yameshatolewa na waziri Mwandosya lakini bado anaendelea. "Nilipopata habari kwamba Mkurugenzi huyu bado hupo, nimewasiliana na Waziri mwenye dhamana, nikamuuliza kwa nini mhandisi huyu bado yupo, anasema alishaagiza aondoke lakini cha kushangaza nasikia bado yupo", alisema Nape.


Nape alisema, ni lazima mhandisi huyo achukuliwe hatua kwa kuwa vitendo vyake vinasabisha wananchi kuichukua serikali na hatimaye lawama hizo huishia kwenye Chama Cha Mapinduzi kilichopewa dhama ya kuunda serikali. "Lakini chuki hizi za wananchi zinazosababishwa na mhandisi kama huyu, hatimaye huishia kwa wananchi hao kuona Chama Cha Mapinduzi si mtetezi wao na hivyo kukinyima kura wakati wa uchaguzi", alisema Nape.

No comments:

Post a Comment