Tuesday, June 14, 2011

BENKI YA KCB TANZANIA YAPANDA MITI 21,000 KUUNGA MKONO UTUNZAJI MAZINGIRA!

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Benki ya KCB Tanzania Christine Manyenye akiwaongoza wafanyakazi wenzake kupanda miti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na ya mazingira duniani iliyofanyika katika Kijiji cha Msongola, Chanika jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Edmund Mndolwa (Kushoto) akipanda mti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na ya mazingira duniani iliyofanyika katika Kijiji cha Msongola, Chanika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo , Moezz Mir na katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Edmund Mndolwa (Kushoto) akimwagilia maji mti alioupanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na mazingira duniani uliofanyika katika Kijiji cha Msongola Chanika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye.

Diwani wa Kata ya Msongola, Angela Malembeka akipanda mti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na mazingira duniani uliofanyika katika Kijiji cha Msongola Chanika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Moezz Mir na katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Christine Manyenye.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakimwagilia maji katika moja ya mti waliyopanda wakati wa wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na mazingira duniani uliofanyika katika Kijiji cha Msongola Chanika jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakigawa juisi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Msongola walioshiriki uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na mazingira duniani uliofanyika katika Kijiji cha Msongola Chanika jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Benki ya KCB Tanzania Christine Manyenye na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Msongola wakimwagilia maji mti walioupanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na mazingira duniani iliyofanyika Kijiji cha Msongola, Chanika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mfanyakazi wa Benki hiyo.

No comments:

Post a Comment