Friday, May 13, 2011

SERIKALI YATIA SAINI UJENZI WA BARABARA YA MINJINGU HADI ARUSHA!

                                               Mafundi wa barabara hiyo wakiwa kazini
Serikali kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), imesaini Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Arusha –Minjingu yenye urefu wa kilomita 98 kwa kiwango cha lami na Mkandarasi SOGEA SATOM, kutoka nchini Ufaransa.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, MHANDISI PATRICK MFUGALE, amesema Mradi huo ambao utafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa asilimia mia moja unatarajiwa kukamilika oktoba, 2013 huku ukitarajia kugharimu zaidi ya bilioni 75.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa SOGEA SATOM, DAVID CURTARELLO, amesema kufuatia kuaminiwa na Serikali, watahakikisha ukarabati wa barabara hiyo unakamilika mapema na kwa kiwango kinacholidhisha.

No comments:

Post a Comment