Friday, May 13, 2011

ALIYEMBAKA BINTI WA MIAKA MINNE JELA MAISHA KIBAHA!

                                                  MAHAKAMA KUU TANZANIA
Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani imemhukumu Emmanuel Peter mkazi wa mtaa wa Misugusugu wilayani humo kifungo cha maisha jela kwa kosa la kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo Bwana MOHAMED SANDUKU ameileza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei 26 mwaka jana baada ya kumrubuni mtoto huyo kwa kumtuma dukani lakini badala yake alimwingiza kwenye jengo linaloendelea kujengwa na kumbaka.


Akitoa hukumu yake hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Kibaha BI BAHATI NDESARUA amesema kitendo alichokifanya mtuhumiwa hakivumiliki ndani ya jamii na ni unyama kwa kumfanyia kitendo hicho mtoto mwenye umri mdogo.

No comments:

Post a Comment