Monday, March 5, 2012

RAIS KIKWETE ALIPOWASILI MJINI MOSHI LEO KWA ZIARA YA SIKU TATU!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa furaha mara alipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hii. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokewa kwa furaha walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hiitayari kwa ziara ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taaria ya Mkoa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama mara tu baada ya kuwasili Ikulu ndogo mjini Moshi jioni hii. PICHA ZOTE NA IKULU.

Na Mwandishi Wetu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Moshi jioni ya leo, Jumapili, Machi 4, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.


Miongoni mwa shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.


Shughuli hiyo itakayofanyika kesho Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)


Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.


Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment