Monday, March 26, 2012

WAZIRI MAIGE ATEUA BODI YA WAKURUGENZI YA BODI YA UTALII!

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel M. Maige (MB) (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawako pichani) juu ya uteuzi wa wajumbe watano kuunda Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii (TTB) kuanzia tarehe 23 Machi, 2012, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Ibrahim Mussa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel M. Maige (MB) kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wajumbe watano kuunda Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii (TTB) kuanzia tarehe 23 Machi, 2012.


Uteuzi huo unafuatia Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete kumteua Balozi Charles A. Sanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTB mapema wiki hii. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi hiyo itakayodumu kwa miaka mitatu ni pamoja na:-

1. Prof. Isaya Jairo PhD, Mhadhiri wa Biashara na Uchumi, Chuo cha Usimamizi wa Fedha, IFM;
2. Ndugu Teddy Mapunda, Mtaalamu wa Masoko (Marketing) na Afisa Uhusiano Serengeti Breweries Limited;
3. Ndugu Samwel D.I. Diah, Mtaalamu na Mdau wa Biashara na Utalii na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Tanzania Travel Co. Limited;
4. Mhe. Kaika S. Telele (Mb), Mbunge wa Ngorongoro na Mdau wa Utalii na;
5. Mhe. Abdulkarim Shah (Mb), Mbunge wa Mafia na Mdau wa Utalii.

No comments:

Post a Comment