Thursday, February 23, 2012

SERIKALI KUSITISHA MFUMO WA ANALOJIA IFIKAPO DISEMBA 31 MWAKA HUU!

                                                                        Analog Signal
Serikali imetangaza kusitisha rasmi mfumo wa matumizi ya Teknolojia ya Analojia ifikapo Disemba 31, mwaka huu ambapo mfumo mpya wa teknolojia ya Digitali utaanza kutumika rasmi Januari Mosi 2013.



Akitangaza uamuzi huo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof MAKAME MBARAWA amesema teknolojia ya Digitali ni mpya na mbadala katika vituo vya utangazaji ambayo imekuja ili kukuza maendeleo ya kiuchumi.
                                                                   Digital Signal

No comments:

Post a Comment