Sunday, January 8, 2012

MNYIKA AMJIBU WAZIRI MAGUFULI KUHUSU NAULI ZA VIVUKO KIGAMBONI!

Na MwanaEastafrica
Mbunge wa Ubungo Jijini Dar es Salaam JOHN MNYIKA amezungumzia tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Waziri wa Ujenzi DK JOHN MAGUFULI wakati akijibu kauli za wabunge wa Dar es Salaam juu ya ongezeko la nauli katika vivuko vya Kigamboni na maeneo mengine nchini.


Akizungumza jijini Dar es Salaam MNYIKA amesema kuwa, akiwa katika kikao hicho binafsi hakupinga ongezeko la nauli kutoka shilingi mia hadi mia mbili bali alipinga ongezeko la bei ya vyombo vinavyovushwa kutumia vivuko vya Magogoni ikiwemo maguta, mikokoteni, baiskeli na magari. Katika maelezo yake akiwa katika mkutano huo wa wabunge alisisitiza kuwa kero ksi kupanda kwa nauli ya mtu mzima bali ongezeko la vyombo hivyo ambapo mwishoni mtumiaji humbebesha gharama zote mlaji.


“Mathalani baiskeli za matairi matatu bei imepanda kutoka shilingi 200 hadi 1800, bei ambayo ni kubwa kuliko ya gari dogo, bajaj zimepanda toka shilingi 300 hadi 1300, mikokoteni imeongezeka toka 200 hadi 1500, naomba viwango vyote vipya cvisitishwe hadi serikali itoe maelezo ya msingi ya agizo hilo,” alisema.
Amesema toka Waziri atoe kauli zisizokuwa na ukweli dhidi yake hakutoa tamko kwa kuwa alikuwa akitekeleza majukumu mbalimbali jimboni mwake.


Mnyika pia amezengumzia upotoshaji uliofanywa na Waziri Magufuli kwamba hajawahi kuzungumzia masuala yanayokihusu kituo kikuu cha Mbasi Ubungo cha 200 na kwamba kama anavyopinga ongezeko holela la vivuko nchini alisahawahi kupinga ongezeko hilo kituoni hapo. “Ukweli ni kwamba viingilio vya kituo kikuu cha mabasi ubungo vilipitishwa kwa kutungiwa sheria ndogo na jiji kabla ya mimi kuchaguliwa kuwa Mbunge. Hata hivyo mara ya kuwa mbunge niliendelea na harakati nilizozianza za kupinga ufisadi wa mapato katika kituo hicho,” aliseama Mnyika.
Mbali na hilo pia alizungumzia kuhusiana na juu ya kupendekeza barabara za jiji kupandishwa hadhi ili zishughulikiwe na serikali kuu kwa ajili ya kupunguza foleni katika jimbo lake Ubungo na Dar es Salaam kwa ujumla.Katika hilo alisema baada ya kuchaguliwa katika kikao chake cha kwanza akiwa mbunge alishiriki kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Dar es Salaam chini ya TANROADS na kupendekeza barabara husika kupandishwa hadhi.


Kuhusu madai ya kushindwa kuja na wazo la kushirikiana na wakala wa nyumba TBA Mheshimiwa ili kutafuta malazi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Mnyika alisema yeye ni mmoja wa wabunge waliochangia harambee ya ujenzi wa mabweni hayo chini ya Rais Jakaya Kikwete. Alisema, ukweli ni kwamba kazi kubwa ya TBA ambayo iko chini ya Wizara ya Waziri Magufuli ni kujenga nyumba za watumishi wa umma na katika mwaka 2011/2012 ina rasilimali chache za kumalizia miradi iliyopo na kutafuta viwanja vya kujenga nyumba za serikali.

“Ingekuwa TBA ina fursa hiyo anayodai Waziri Magufuli angeiwezesha kuwepo katika harambee iliyofanywa na Rais Kikwete jimboni Ubungo kwa ajili ya Kituo cha Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM ambapo watu na taasisi mbalimbali zilijitokeza kuchangia,” alisema Mnyika.

No comments:

Post a Comment