Tuesday, November 1, 2011

WATANZANIA WAOMBWA KUENDELEA KUUPIGIA KURA MLIMA KILIMANJARO!

Watanzania nchini wametakiwa kushiriki katika kulitangaza taifa kwa kuupigia kura Mlima Kilimanjaro ili uingie katika maajabu saba ya Dunia ili uweze kupata nafasi ya kuwa kivutio kwa watalii wengi watakao ingia nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii GEOFREY TENGENEZA amesema kupitia sekta ya utalii wa ndani, Mlima Kilimanjaro utasaidia kuleta maendeleo na kuinua uchumi wa nchi kwa kasi iwapo watanzania watashiriki katika zoezi hilo kikamilifu kwa kutumia simu zao za mkononi.
                                                             Hongera kwa kufika kileleni.

No comments:

Post a Comment