Tuesday, November 1, 2011

WANAKIJIJI NKOLOLO BARIADI SHINYANGA WAMSHAMBULIA KWA MAWE HADI KUMUUA MGANGA WA KIENYEJI!

Wananchi wa kijiji cha Nkololo, Wilaya ya Bariadi, Mkoani Shinyanga wamemshambulia kwa mawe Bw SEIF HAMAD ambaye ni mganga wa kienyeji na kumsababishia kifo chake kwa madai kuwa alitaka kumchuna ngozi Bw MBISHI TANO mkazi wa kijiji hicho.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga DIWANI OTHUMANI amesema kuwa tukio hilo limetokea katika kijiji hicho majira ya saa nne asubuhi ambapo inadaiwa kuwa mganga huyo alikamatwa baada ya kutaka kufanya unyama huo na kuanza kushambuliwa na wanainchi wenye hasira kali.


Aidha kamanda DIWANI amewata wananchi wa mkoa huo kutojichukulia sheria mikononi na badala yake matukio kama haya wayalipoti katika vyombo vya sheria ili sheria ifate mkondo wake.

No comments:

Post a Comment