Tuesday, November 1, 2011

TIGO YAKABIDHI RAMBIRAMBI KWA WATEJA WAO WALIOFIWA KUPITIA TIGO BIMA!

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na kampuni ya Bima GOLDEN CRESCENT na MICRO ENSURE, imekabidhi hundi ya malipo ya fidia ya rambirambi ya shilingi laki sita kwa wateja wawili baada ya kupoteza wa wazazi wao.

Mwakilishi wa Tigo Bima, JOE BENDERA amesema huduma ya bima inawapa fursa wateja kupata msaada wa kifedha unapoitajika ambapo Kampuni hiyo inatoa huduma ya bima rahisi.


Kwa upande wake JOSEPH ZACHARIA ambaye amefidiwa baada ya kumpoteza baba yake aliyefariki ametoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuonyesha ahadi ya kweli.

No comments:

Post a Comment