Tuesday, November 1, 2011

MGAO WA UMEME BADO WAENDELEA KUWA KERO KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI!

Licha ya Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO kutangaza kumalizika kwa mgao wa umeme kuanzia mwezi Octoba hadi Decemba mwaka huu bado hali hiyo imeonekana kuendelea kuwa kero katika baadhi ya maeneo Jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi Jijini, wamesema kuwa tatizo la mgao wa umeme kwa sasa limekuwa kubwa zaidi huku wakilitupia lawama shirika hilo kufuatia kutoa taarifa ya kumalizika kwa tatizo hilo.


Kwa upande wa uongozi wa shirika hilo ulieleza kuwa tatizo la kukatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo Jijini kunasababishwa na hitirafu za kiufundi.

No comments:

Post a Comment