Tuesday, November 1, 2011

UMOJA WA MASHIRIKA YA KIDINI NCHINI IRCPT WAWAOMBA WATANZANIA KUWA WAVULIVU WAKATI WA MCHAKATO UUNDWAJI KATIKA MPYA!

Umoja wa Mashirika ya Kidini nchini ( IRCPT), umewataka Watanzania kote nchini kuwa wavumilivu katika mchakato wa uundaji wa katiba mpya kutokana na zoezi hilo kuhitaji muda wa kutosha katika utekelezaji wake.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili mwenendo na ushiriki wa umoja huo katika uundwaji wa katiba mpya, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Shekh. FADHIL SULEIMAN SORANGA, amesema kuwa kutokana na mchakato huo kuhusisha wadau mbalimbali kuchangia maoni yao zikiwemo taasisi za dini utafanikiwa kwa kiasi makubwa.


Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa IRCPT, Padre. ANTONY MAKUNDE, amesema mawazo na maoni yaliyotolewa awali na viongozi wa dini pamoja na taasisi balimbali wakati wa uwasilishwaji wa mswaada wa katiba bungeni yamekidhi malengo yake na kuwa zoezi la uundaji wa katiba mpya lipo katika hatua nyingine.

No comments:

Post a Comment