Sunday, November 27, 2011

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JIONI YA LEO NOVEMBA 27, 2011

                 Ujumbe wa Chadema ukiingia Ikulu tayari kwa mazungumza na Rais Jakaya Kikwete.
Hapa ujumbe huo, ukisubiri kuonana na Rais Jakaya Kikwete.Mh Mbowe anaonekana akifurahia.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Taifa Chadema Freeman Mbowe leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
                      Rais Jakaya Kikwete akiwa tayari kuzungumza na ujumbe huo wa Chadema
Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe akiomba hudhuru wa kuondoka kwenda kwenye mazishi ya maaskofu waliokufa ajalini. Mazishi yao yamefanyika Pugu.
           Hapa Rais Jakaya Kikwete akigana na Mbowe mara baada ya mazungumzo yao Ikulu leo
    Tundu Lissu naye alikuwepo, Hapa akisalimiana na William Lukuvi, kwa nyuma ni Prof Baregu.
  Hii ilikuwa ni picha ya pamoja baada ya mazungumzo yao kuhusiana na uundwaji wa katiba mpya.
Haya ni baadhi ya mapendekezo yetu, tafadhali Mh Rais yapitie na utupe mapendekezo yako.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa JAKAYA KIKWETE amekutana na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ili kujadiliana kuhusiana na mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania.

Rais Kikwete amekubali kukutana na ujumbe wa Chadema kama sehemu sehemu ya maamuzi yake ya kuhakikisha kuwa mchakato huo unaongozwa na mashauriano mapana zaidi miongoni mwa wadau mbali mbali.


Wakati wa mazungumzo yao, Rais Kikwete aliuhakikishia ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Bw FREEAM MBOWE kuwa atasikiliza ushauri wao ikiwemo kuufanyia marekebisho muswaada wa uundwaji katiba mpya kwa maslahi ya taifa.


Mkutano huo uliofanyika Ikulu unafuatia uamuzi wa Rais Kikwete kukubali ombi la uongozi wa Chadema la kukutana naye kuhusu mchakato huo. Muswada wa Sheria hiyo ulipitishwa na Kikao cha Bunge kilichomalizika hivi karibuni mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment