Tuesday, November 8, 2011

CHADEMA YALAANI JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU DHIDI YA VIONGOZI WAKE!

Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kimelalamikia kitendo cha jeshi la polisi nchini kutumia nguvu kuwakamata viongozi wao na kuwapiga wanachama wao waliokusanyika kuhudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya NMC jijini Arusha hapo jana.

Akizungumzia tukio hilo hii leo katibu mtendaji ofisi ya katibu mkuu Bwana VICTOR KIMESERA amesema uongozi wa chama hicho kwa sasa umeishiwa imani na jeshi la polisi hivyo wamekusudia kukaa kikao maalum cha kujadili suala hilo.


Naye mwenyekiti wa Baraza la vijana wa chama hicho Bwana HECHE JOHN amekanusha tuhuma kwamba chama hicho kinahamasisha vurugu.

No comments:

Post a Comment