Thursday, October 20, 2011

UN YAENDESHA MJADALA WA HADHARA JIJINI DAR ES SALAAM!

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akizungumzia msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la Libya wakati alipokuwa akifungua mjadala wa hadhara ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa uliofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya 66 siku ya Umoja wa Mataifa. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akifafanua mifumo na mikakati ya Umoja wa Mataifa kwa nchini zinazoendelea wakati wa mjadala huo. Kushoto ni Mhe. Membe.
Wazungumzaji waalikwa kutoka kushoto Mwendesha Mjadala Bw. Hamza Kasongo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa-TZ Alberic Kacou na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dr. Bohela Lunogelo.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasomi waliohudhuria mjadala wa hadhara ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa uliofanyika leo jijni Dar es Salaam.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasomi waliohudhuria mjadala wa hadhara ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa uliofanyika leo jijni Dar es Salaam.
Na Eastafrica Bloger

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umeandaa mjadala wa wazi ulioshirikisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu jijini Dar es Salaam huku serikali ya Tanzania ikiwakilishwa na Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe.



Wazungumzaji waalikwa katika mjadala huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee pamoja na Waziri Membe ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alberic Kacou, Mkurugenzi Mtendaji wa wa Economic and Social Research Foundation- ESRF Dakta H. Bohela Lunogelo huku Msimamizi Muongozaji wa mjadala huo akiwa ni Mzee Hamza kasongo. Mada kuu ulikyokuwa ikijadiliwa katika mjadala huo ni ‘Miaka 50 kuanzia sasa: Mashirika ya Kimataifa yana majukumu katika siku za usoni hapa Tanzania?.


Mjadala huo umeanza kwa Waziri Membe kutoa msimamo wa Tanzania kuhusu vita vinavyoendeleoa nchini Libya huku Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alberic Kacou akifafanua mifumo ya Umoja wa mataifa ikifuatiwa na maswali kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na taasisi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment