Thursday, October 6, 2011

MLEMAVU FRIDA KAVISHE AKABIDHIWA FEDHA TASLIMU 800,000/- ZILITOLEWA NA MSAMALIA MWEMA ILI AKAJIUNGE NA MASOMO YA SHAHADA YA UCHUMI MNMA!

Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds Media Group Ltd BI JOYCE SHEBE akiwa ameshikilia kiasi cha fedha taslimu shilingi 800,000/- zilizotolewa na msamalia mwema tayari kumkabidhi Mlemavu Frida Kavishe kwa ajili ya kulipia ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Kutoka Kulia ni kaka wa Frida, Omari Mkete na Mhariri wa Habari Clouds FM/TV Bw Lazaro Matalange.
Bi Frida Kavishe mlemavu anayetarajia kujiunga na Shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akiwa na kaka yake Omari Mkete nje ya Ofisi za Clouds Media Group Ltd tayari kupokea msaada wa fedha taslimu shilingi 800,000/- zilizotolewa na msamalia mwema ili akalipie ada.
Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds Media Group Ltd BI JOYCE SHEBE akimkabidhi kiasi cha fedha taslimu shilingi 800,000/- zilizotolewa na msamalia mwema kwa Mlemavu Frida Kavishe alizoomba kwa ajili ya kulipia ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Anayeshuhudia ni kaka wa Frida, Omari Mkete.
Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds Media Group Ltd BI JOYCE SHEBE akizungumza baada ya kukabidhi kiasi cha fedha taslimu shilingi 800,000/ zilizotolewa na msamalia mwema kwa Mlemavu Frida Kavishe (Kushoto) kwa ajili ya kulipia ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Katikati ni kaka wa Frida, Omari Mkete.
Mlemavu Frida Kavishe (Kushoto) akimshukuru mungu baada ya kukabidhiwa kiasi cha fedha taslimu shilingi 800,000/ zilizotolewa na msamalia mwema kwa ajili ya kulipia ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Kulia ni kaka wa Frida, Omari Mkete.
Baadhi ya watendaji wa chumba cha habari Clouds FM/TV kutoka kushoto Shaffih Dauda, Sophia Kessy, Jackie Kombe, Joyce Shebe, Jerome Risasi na Juma Katunda wakiwa kwenye picha ya pamoja na Frida Kavishe na Omari Mkete mara baada ya makabidhiano ya fedha hizo.

No comments:

Post a Comment