Wednesday, September 7, 2011

WAJUE WALIOPATA VIBALI VYA VITALU VYA UWINDAJI KWA MWAKA 2013 HADI 2018!

Wizara ya Maliasili na Utalii inataarifu umma kuwa mchakato wa kupitia maombi ya vitalu kwa kipindi cha 2013 – 2018 umekamilika na kuwa kampuni 60 zitagawiwa vitalu. Kampuni zitakazogawiwa vitalu ni kwa uwiano ufuatao:

i. Kampuni za kitanzania zitakazogawiwa vitalu ni 51 kati ya 60 (sawa na asilimia 85% ya kampuni zote);
ii. Kampuni za kigeni zitakazogawiwa vitalu ni 9 kati ya 60 (sawa na asilimia 15% ya kampuni zote);
iii. Kampuni 15 zitapewa kitalu kimoja kwa kuzingatia maombi yao. Kati ya kampuni hizo, kampuni 1 ni ya kigeni (sawa na asilimia 2% ya kampuni zote) na 14 ni za kitanzania (ambayo ni asilimia 23% ya kampuni zote);
iv. Kampuni zenye vitalu vingi, yaani vitalu 4 hadi 5 ni 13, ambayo ni sawa na asilimia 22% ya kampuni zote);
Aidha, kuna vitalu 14 ambavyo havijapata waendeshaji, 10 havijaombwa kabisa hata baada ya kutangazwa mara ya pili, na 4 vimeombwa mara zote mbili na waombaji wasio na sifa kabisa kisheria.

Hivyo, serikali inatafakari namna ya kuviendeleza na kuviendesha vitalu hivyo ambavyo vingi rasilimali zake zimepungua sana kutokana na uvamizi wa wananchi kwa shughuli za kilimo, makazi na hata ufugaji. Kwa kuwa Kampuni za uwindaji za kigeni, kwa mgao huu, tayari zimeshafikia ukomo wa asilimia 15%, hii ni fursa kwa wawekezaji wapya, hasa watanzania kuleta maombi vitalu hivyo vitakapotangazwa.
 2.0 SHERIA ILIYOTUMIKA
Wizara ya Maliasili na Utalii, Idara ya Wanyamapori, pamoja na mambo mengine, imekuwa ikisimamia matumizi ya wanyamapori ambayo ni matumizi ya uvunaji (consumptive utilization) na matumizi yasiyo ya uvunaji (non consumptive utilization) kupitia kifungu 38 cha sheria ya Wanyamapori na.5 ya Mwaka 2009 (sura 283). Mojawapo ya matumizi ya uvunaji ni Biashara ya Uwindaji wa kitalii, biashara ambayo imekuwa katika uendeshaji na usimamizi wa sheria tofauti tangu 1934.


Usimamizi wa Biashara ya Uwindaji wa kitalii kwa muda mrefu umekuwa ukifanywa zaidi na Makampuni ya kigeni na wateja wao wengi walitoka nje. Kabla ya sheria mpya, sheria Na.12 ya mwaka 1974 na kanuni zake ndizo zilizokuwa zikitumika. Hata hivyo, kumekuwepo mapungufu kadhaa katika mfumo uliokuwa ukitumika ambao ulisababisha malalamiko mengi toka kwa wadau wa sekta hii. Hivyo, sheria ya Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 ililenga kurekebisha mapungufu hayo.


Kufuatia matakwa hayo ya kisheria, maandalizi yafuatayo yalifanyika kati ya 2008 hadi Januari 2011:-
i. Kupitia upya vitalu vyote kwa lengo la kuvigawanya ili kuongeza washiriki na mapato kwa kuzingatia ukubwa, ubora (kama vile wingi na aina za wanyama, uwepo wa maji na malisho, miundombinu ya eneo). Kazi hii ilifanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na kukamilika Desemba 2010.
ii. Kuandaa kanuni zitakazoweka, pamoja na mambo mengine, vigezo vitakavyotumika kufanya tathmini kwa waombaji wa vitalu. Kazi hii ilikamilika Julai 2010.
iii. Kuteua wajumbe wa kamati, kazi ambayo ilikamilika Machi 2011. Wajumbe wafuatao waliteuliwa kwa mujibu wa Kifungu 38 (3) cha Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya 2009:-

Na Mjumbe Sifa kisheria Sifa Binafsi

1 Bakari Mbano - Mwenyekiti Mhifadhi Alikuwa Mkurugenzi Wanyamapori 1995 - 1998, 2 Dkt. Simon Mduma Mkurugenzi Mkuu TAWIRI- Mjumbe Mhifadhi Mhifadhi, mtafiti, 3 Edward Msyani (kwa niaba Mkuu wa Chuo) MWEKA - Mjumbe Mhifadhi Mhifadhi, 4 Saidi Nzori – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu -Mjumbe Mwanasheria Ameshiriki kwenye mchakato wa sheria na. 5 ya 2009, anaijua vema., 5 Allan Kijazi - Mkurugenzi Mkuu TANAPA-Mjumbe Mhifadhi Mhifadhi, 6 Obed Mbangwa - Mkurugenzi wa Wanyamapori - Katibu Mhifadhi Mhifadhi, Mkurugenzi wanyamapori, 7 Mhe. Steven Ihema Sheria, biashara Alikuwa Kamishna wa maadili, Jaji Mstaafu, 8 Mhe. Mary Mwanjelwa Biashara, jinsia Mbunge, mtaalamu wa uwezeshaji na biashara, 9 Prof. Letisia Rutashobya Biashara, jinsia Mhadhiri mwandamizi Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, 10 Ndugu Dan Nsanzugwanko Biashara Amekuwa Naibu waziri Kazi, anajua Biashara na uwezeshaji, 11 Ndugu Beno Malisa Sheria, biashara Mwanasheria
3.0. MCHAKATO ULIVYOKUWA
Zoezi zima la ugawaji vitalu lilitangazwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Ezekiel Maige (MB), katika mkutano wake na waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Habari Maelezo tarehe 04 Februari 2011.
Matangazo rasmi ya kukaribisha waombaji wa vitalu yalitolewa kwenye magazeti ya Majira, Uhuru, Daily News, Guardian na Habari Leo ya tarehe 10 Februari 2011 na tarehe 20 Juni 2011.


Aidha, matangazo yaliwekwa pia kwenye ubao wa matangazo wa Wizara na kwenye Tovuti ya Wizara: http://www.mnrt.go.tz. Jumla ya waombaji 91 walijitokeza baada ya tangazo ya Februari 2011 na waombaji 17 walijitokeza baada ya tangazo la Juni 2011.


Waombaji wote, baada ya kulipia maombi yao benki kupitia akaunti ya Wizara, walifika ofisi za Wizara Arusha na Dar es Salaam wakiwa na pay-in-slips walizolipia benki, kuchukua fomu za maombi na kusaini kwenye “register” maalum iliyoandaliwa kwa ajili hiyo, aidha, waliandika tarehe ya kuchukua fomu. Baada ya kujaza fomu, walizirejesha, pamoja na viambatisho vyote vilivyohitajika kwa mujibu wa fomu na kuzikabidhi ofisi za Wizara Dar es Salaam na kusaini tena kwenye “register” na kuandika tarehe ya fomu kupokelewa. Hii ni kuzingatia matakwa ya kanuni kwamba maombi yote yapokelewe ndani ya siku 30 kuanzia siku ya tangazo.


Waombaji wote waliarifiwa kwamba watatembelewa na Kamati, na baadaye walitembelewa na Kamati kwa mahojiano na taarifa zao za kina. Kamati ilifanya kazi kwa siku 60 kwa kila awamu na kuwatembelea waombaji wote nchi nzima. Waombaji walipewa alama kwa kuzingatia ‘nyaraka zilizowasilishwa na maoni ya kamati baada ya kuwatembelea’.


Alama zilitolewa kwa vigezo vifuatavyo:- i. Kuwa na vifaa vya kazi au bondi ya TShs 1bn kwa wageni na TShs 300m kwa watanzania; ii. Mpango wa biashara (business plan); iii. Nyaraka zinazothibitisha uhalali wa kisheria wa kampuni kama TIN, Certificate of Incorporation, MoU na Articles of Association, VAT registration number nk; iv. Historia ya Biashara ya mwombaji ikiwemo ulipaji wa kodi mbalimbali za serikali na tozo za Wizara/Idara na ushiriki wake katika kuchangia jamii jirani na kuzuia ujangili (kwa waombaji wa zamani); v. Kuzingatia matakwa ya sheria ya Wanyamapori, hasa kwa wageni kwa mfano, kuwa na “Professional hunters” ambao ni Watanzania; kuwa na wanahisa watanzania wenye hisa zisizopungua 25% ya hisa zote. Kamati iliweka alama 50 kama alama ya chini kabisa ambayo mwombaji anatakiwa apate ili kupendekezwa kugawiwa kitalu.
4.0. KAMPUNI ZILIZOGAWIWA VITALU
Kampuni zilizopewa kipaumbele katika ugawaji wa vitalu ni zile zenye sifa zifuatazo:- i. Kampuni ambazo zimewekeza sana kwenye sekta katika:-

a) Ulipaji kodi za serikali;, b) Ulipaji wa tozo mbalimbali za vitalu na nyara kwenye Idara; c) Kuchangia jitihada za Wizara katika kupambana na ujangili;, d) Kutengeneza miundombinu kama barabara na kambi za wageni hifadhini au kwenye vitalu vyao;, e) Uchangiaji miradi ya maendeleo kwa jamii zinazoishi jirani na hifadhi;, f) Kujitangaza kwenye masoko hasa Marekani na ulaya (ambayo huleta wageni zaidi ya 95% ya wageni wote). ii. Kampuni mpya ambazo zimeonyesha mpango mzuri wa biashara na kuthibitisha uwezo wa kifedha, kiutaalamu na kimasoko katika kumudu biashara husika;, iii. Waombaji wenye sifa ambao ni waombaji pekee kwenye maeneo waliyoomba. Kwa kuzingatia hayo, kampuni zilizogawiwa vitalu kwa muhula wa uwindaji 2013-18 ni hizi zifuatazo:
NO. JINA LA KAMPUNI URAIA
1. Marera Lodges and Tours ltd Tanzania, 2. Bunda Safaris ltd Tanzania, 3. Siafu safaris ltd Tanzania,
4. SNF Hunting safaris ltd Tanzania, 5. Traditional African Safaris ltd Tanzania, 6. Fereck Safaris Limited Tanzania, 7. Miombo safaris ltd Tanzania, 8. Tanzania Bundu Safaris Tanzania, 9. Royal Frontiers ltd Tanzania, 10. Game Frontiers ltd Tanzania, 11. Northern Hunting Ent. Ltd Tanzania, 12. Western Frontiers ltd Tanzania, 13. Mkwawa Hunting Safaris ltd Tanzania, 14. EBN Hunting Safaris Ltd Tanzania, 15. Tanza Guides ltd Tanzania, 16. African Buffalo Safari Trackers ltd Tanzania, 17. Tanzania Wildlife Co ltd Tanzania
18. Old Nyika Safaris ltd Tanzania, 19. Muhesi Safaris ltd Tanzania, 20. Z. H. Poppe ltd Tanzania, 21.
Kilimanjaro Game Trails Tanzania, 22. Michael Matheankis Safaris Tanzania, 23. Safari Royal Holding Tanzania, 24. Tandala Hunting Safaris Tanzania, 25. Go WildHunting Safaris Tanzania, 26. Bushman Hunting Safaris Tanzania, 27. Melami Hunting Safaris Tanzania, 28. Mwatisi Safaris Tanzania, 29. Tanganyika Game Fishing Tanzania, 30. Masaailand Hunting co Tanzania, 31. Safari Club ltd Tanzania, 32. Kiboko Hunting Safaris Tanzania, 33. Pori Trecker safaris of Africa Tanzania, 34. Green Miles ltd Tanzania, 35. Rungwa Game Safaris Tanzania, 36. East Africa Trophy Hunters Tanzania, 37. Kilombero North Safaris Tanzania,
38. Wembere Hunting Safaris Tanzania, 39. Coastal Sable Safaris Tanzania, 40. Eshkesh Safaris Tanzania
41. Palahala Safaris & Horizon Tanzania, 42. Maully Tours & Safaris Tanzania, 43. Giant Hunting club ltd Tanzania, 44. Mwanauta Co ltd Tanzania, 45. Wild Foot Prints ltd Tanzania, 46. Malagalasi Hunting Safaris ltd Tanzania, 47. African Trophy Hunting ltd Tanzania, 48. HSK Safaris co ltd Tanzania, 49. Green Leaf ltd Tanzania, 50. Out of Africa Safaris Tanzania, 51. Said Kawawa Hunting Safaris Tanzania, 52. Tanganyika Wildlife Safaris Co ltd Nje, 53. Barlette Safaris Corp ltd Nje, 54. Gerald Pasanisi Safaris Corp Nje,
55. Tanzania Game Traker Safaris Nje, 56. Wengert Windrose Nje, 57. Grumeti Reserves Nje,
58. Robin Hurt Safaris Nje, 59. Otterlo Business Corp Nje, 60. Luke Samarasi Safaris Nje.
5.0. HITIMISHO
Wizara ya Maliasili na Utalii inawashukuru wadau wote kwa ushirikiano waliouonyesha wakati wa mchakato huu. Tunawashukuru sana watanzania na wageni waliojitokeza kutaka kufanya biashara hii. Hata hivyo, kwa vyovyote vile, pale ambapo vitalu ni vichache kuliko waombaji, lazima watakuwepo watakaopata na watakaokosa.


Wengi wa waliokosa wanazo sifa, hivyo tunawaomba wasikate tamaa, kwani sheria ya sasa inatutaka kumnyang’anya mwendesha kitalu wakati wowote akikiuka taratibu. Hivyo wakati wowote tunaweza kuwahitaji kibiashara.


Kwa watanzania ambao wengi wamepata ni vema waelewe kwamba mazingira ya biashara hii kwa sheria ya sasa ni tofauti na zamani. Hivyo waitumie nafasi hii kuonyesha uwezo wao na kujijengea uzoefu. Wanatakiwa wasifanye biashara kwa kutafuta faida pekee bila uwekezaji na uadilifu. Biashara hii inahitaji uwekezaji mkubwa na kujitangaza sana. Pia inahitaji uadilifu hasa kwa serikali na wageni. Wageni wengi wanakuja kwa ‘kuaminiana’ na kampuni zinazowapokea na kuwawindisha.


Kwa mujibu wa sheria, Wizara itawaandikia barua washiriki wote, waliopata na wasiopata, kuwataarifu kuhusu ya maamuzi haya. Taarifa hii inapatikana pia kwenye tovuti ya Wizara ya Maliasili na Utalii www.mnrt.go.tz.

No comments:

Post a Comment