Sunday, September 18, 2011

VODACOM TANZANIA YAFIKISHA WATEJA MILIONI 10!

Vodacom Tanzania inapenda kuwashukuru sana watanzania wote na hasa wateja wetu kwa kuendelea kushirikiana nasi hadi hivi sasa tumefikisha wateja milioni 10. Tuna kila sababu ya kuendelea kuwashukuru wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla kwa uaminifu na mchango wao mkubwa wanaoendelea kuuonyesha kwetu kwa kipindi chote cha miaka 11 sasa.


Mafanikio mbalimbali tuliyoyapata hadi hivi sasa ni matokeo ya kuelewa mahitaji muhimu ya wateja wetu na kuhakikisha kuwa tunayatimiza na kuwafanya wateja wetu waendelee kufurahia huduma zetu. Kama tulivyowaahidi wakati wa mabadiliko ya muonekano wetu, tunapenda kuwasisitizia kuwa tutaendelea kuyatimiza yale yote tuliyowaahidi na kuyaboresha zaidi.


Vilevile, tunawahakikishieni kuwa tutaendelea kuwa mtandao ulio bora na unaotoa huduma na bidhaa za bei nafuu zaidi hapa nchini. Ripoti ya idadi ya wateja kama ilivyotolewa na TCRA


Mtandao Vodacom Wateja 10,000,000, Airtel Wateja 5,927,417, Tigo Wateja 4,671,263, Zantel Wateja 1,354,098, TTCL Wateja 226,153, Sasatel Wateja 8,498 na Benson Wateja 2,074

                                     Ahsante Tanzania. Vodacom, kazi ni kwako.

No comments:

Post a Comment