Tuesday, September 6, 2011

MECKY SADICK AWAAMBIA WANAOVAMIA VIWANJA VYA SHULE OLE WAO!


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewataka wananchi waliovamia maeneo ya mipaka ya shule mbalimbali kuondoka mara moja ili kuacha nafasi kwa shule hizo kuendeleza ujenzi wa madarasa mengine.

Akizungumza katika ziara aliyoianza katika Wilaya ya Kinondoni Katika Shule ya Sekondari Kiluvya jijini Dar es salaam, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam SAIDI MECKY SADIKI amesema mipaka ya shule iheshimiwe na itumike katika utaratibu ambao serikali imejipangia katika kuendeleza ujenzi mbalimbali katika shule za serikali na sio kuvamia maeneo hayo.

Aidha Mkuu wa shule ya sekondari ya Kiluvya, FRANCO MAVUNDE amesema changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na ukosefu wa uzio wa shule hasa kwenye swala la nidhamu ambapo wanafunzi wamekuwa wakichelewa kufika shuleni hivyo kupelekea walimu kushindwa kufundisha somo la kwanza kwasababu ya kuchelewa kwa wanafunzi hao.

No comments:

Post a Comment