Thursday, September 22, 2011

DKT BILAL MGENI RASMI UTIAJI SAINI MKATABA WA MIRADI YA MAKAA YA MAWE YA MCHUCHUMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Septemba 21, 2011.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Christant Mzindakaya, nje ya ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam leo Septemba 21, baada ya kumalizika kwa zoezi la kutiliana saini mkataba wa ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Septemba 21, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hngda Corporation Ltd, Liu Canglong, baada ya kuhudhulia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, uliofanyika leo septemba 21 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, baina ya Shirika la maendeleo ya Taifa (NDC) na kamuni hiyo kutoka nchini China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Bendera maalum ya kumbukumbu ya watu wa China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, Liu Canglong, (kushoto) wakisainiana mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Septemba 21, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China, uliofanyika kwenye ukumbu wa Mlimani City Dar es Salaam, leo Septemba 21.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi.

No comments:

Post a Comment