Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban Simba na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad saul, wakiwa pamoja wakati wakisubiri muda wa swala kabla ya kupata futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Meck Dadick, wakiomba dua kwa pamoja baada ya kupata futari iliyoandaliwa na mwenyeji wao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika makazi yake Oysterbay jijini jana, Agosti 27.Rais Dkt. Jakaya kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiagana na baadhi ya wananchi waliofika katika futari iliyoandaliwa na mwenyeji wao Makamu wa rais katika makazi yake Yosterbay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27, ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru kwa kuhudhulia hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban Simba, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu katika makazi yake Oysterbay Dar es Salaam jana Agosti 27.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya CXC Africa Ltd, Charles Hamkah, wakati alipowaalika wageni katika hafla ya futari katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, baada ya hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika makazi yake oystebay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27.Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
No comments:
Post a Comment