Tuesday, August 23, 2011

PHILLEMON LUHANJO AMRUDISHA DAVID JAIRO KAZINI!

PHILLEMON LUHANJO
                                                                  DAVID JAIRO
Serikali imetoa ripoti ya uchunguzi wa awali kuhusiana na tuhuma zilizotolewa dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, DAVID JAIRO, na kubainisha kuwa uchunguzi huo haukupata uthibitisho dhidi ya tuhuma hizo.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, mapema hii leo, Katibu Mkuu Kiongozi, PHILLEMON LUHANJO, amesema kufuatia kutothibitika kwa tuhuma kuwa katibu Mkuu huyo amehonga wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2011/2012, ameamuru arejee kwenye majukumu yake ifikapo Agosti 24 mwaka huu.


Akisoma Ripoti hiyo, Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali, LUDOVICK UTOH, amebainisha kuwa ukaguzi maalumu haukupata uthibitisho wa kuwepo kwa Taasisi 20 zilizotakiwa kuchangia bajeti hiyo bali ni Taasisi 4 tu zilizoko chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

No comments:

Post a Comment