Tuesday, August 23, 2011

MBUNGE MTEULE BARAZA LA WAWAKILISHI MH MUSSA KHAMIS SILIMA AFARIKI DUNIA!


                           Mheshimiwa Musa Khamisi Silima akifikishwa Hospitali ya Muhimbili.
Mbunge Mteule kutoka Baraza la wawakilishi Zanzibar, Musa Khamisi Silima, amefariki dunia leo asubuhi, katika hospitali ya taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.

Mbunge Silima alipatwa na ajali ya gari iliyotokea mwishoni mwa wiki, eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma, iliyopelekea pia mkewe Mwanaheri Fahari kufariki dunia papo hapo siku ya tukio, huku dereva wao akijeruhiwa vibaya.

Kufuatia taarifa hiyo, spika wa bunge ameahirisha shughuli zote za bunge kwa ajili ya msiba huo mzito.
                         Hili ndilo gari lililokatisha maisha ya Mheshimiwa Musa Khamisi Silima.

No comments:

Post a Comment