Sunday, July 24, 2011

ZIARA YA NAPE MOSHI MKOANI KILIMANJARO KATIKA PICHA!

Baadhi ya wanachama wapya wa CCM tawi la Chuo Kikuu cha Tumaini, (SIMCO) Moshi mkoani Kilimanjaro, wakiwa kwenye mkutano na Nape mjini HIMO, wapili kulia ni Rais wa Chuo Kikuu cha Tumaini (SIMCO) Moshi, Paul Raurent

KATIBU wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Silo Swai katika mapokezi yaliyofanyika Chekereni mkoani humo. Kushoto ni Katibu wa mkoa Stephen Kazidi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape akimkabidhi kadi ya CCM Simon Ndemela, wakati alipotoa kadi za Chama kwa wanachama wapya 108 wa CCM baada ya kuzindua rasi tawi la wanachama wa CCM kutoka SIMCO , katika mkutano uliofanyika mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea saluti kutoka kwa kijana wa CCM wakati wa mapokezi ya msafara wake, eneo la Chekereni, Vunjo mkoani Kilimanjaro. Wengine ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kili, Silo Swai na Katibu wa mkoa steven Kazidi.
Katibu wa NEC CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza baada ya kuzindua tawi la wanachama wa CCM la wasomi wa Chuo Kikuu cha Tumaini (SIMCO), katika mkutano uliofanyika katika mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro, jana. Wengine kutoka kushoto, wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo Swaijaro na kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kaidi na Mwenyekiti wa Tawi hilo Mijo Laizer
Wanachama wapya wa CCM tawi la SIMCO wakila kiapo baada ya kupewa kadi na Nape mjini Himo, jumla ya wanachama 108 ktoka chuo hicho walikabidhiwa kadi.

No comments:

Post a Comment