Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Mkuki, katika Mnara wa Mashujaa mahala walipozikwa Mashujaa 101 waliopigana vita Msumbiji, ikiwa ni siku ya sherehe ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja hivyo vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wake wa pili, Balozi Seif Ali Idd, wakitembelea na kukagua makaburi ya Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa iliyoadhimishwa katika viwanja vya makaburi ya Mashujaa Naliendele, mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Balozi Seif Ali Idd, wakitembelea na kukagua makaburi ya Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Mashujaa iliyoadhimishwa katika viwanja vya makaburi ya Mashujaa Naliendele, mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe hizo.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakitembelea Chumba cha Makumbusho cha Mashujaa kilichopo katika Viwanja hivyo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment