Monday, July 18, 2011

KAMPUNI YA ALMASI YA PETRA DIAMOND YABAINIKA KUTOLIPA KODI!

                                            HAMAD RASHID MOHAMED (Kushoto)
Kampuni inayomiliki mgodi wa almasi wa Mwadui Shinyanga ya Petra Diamond imebainika kutolipa kodi tangu ilipoanza kufanya kazi zake hapa nchini licha ya kiwango cha mauzo kuongezeka.

Mbunge wa Wawi CUF HAMAD RASHID MOHAMED amesema Bungeni mjini Dodoma kwamba mbali ya kutolipa kodi hiyo serikalini kampuni hiyo pia imepewa mkataba wa muda wa kusafirisha almasi kwenda mnadani bila kuchambuliwa na wataalam wa Kitanzania.


Mgodi huo wenye ukubwa wa hekta za mraba 146, ni moja kati ya migodi mikubwa kabisa inayomilikiwa na kampuni ya Williamson ambapo Petra wanahisa asilimia 75, huku serikali ya Tanzania inahodhi asilimia 25 za mgodi huo.

No comments:

Post a Comment