Tuesday, June 21, 2011

WIZARA YA ELIMU YAOMBWA KUWEKEZA KUCHAPISHA VITABU VYA WALEMAVU!

                                 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Prod Hamis Dihenga
Serikali kupitia Wizara ya Elimu imeombwa kuwekeza katika uchapishaji wa vitabu vyenye maandishi makubwa sanjari na Madaftari yenye mistari mikubwa ili kuondokana na tatizo la uoni hafifu wanalokabiliwa nalo jamii ya walemavu wa ngozi hapa nchini.

Mkurugenzi wa Shirika la Under The Same Sun, VICKY MTETEMA amesema hali ya kutoona vizuri kwa walemavu wa ngozi inapelekea kushindwa kufanya vizuri darasani hivyo serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba Shule zote zinakuwa na ubao mweusi utakaowawezesha wanafunzi hao kuona vizuri.
Aidha kwa upande wa walemavu hao wameelezea adha mbalimbali wanazozipata kwa kushindwa kuona vizuri maandishi kipindi wanapokuwa katika masomo yao darasani.
Shirika hilo limefanikiwa kutoa ufadhili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wapatao 318 kutoka ngazi za chekechea mpaka ngazi ya Uzamili katika Vyuo mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment