Tuesday, June 21, 2011

MPANGO WA STEP AHEAD ULIOBUNIWA NA BENKI YA BARCLAYS KUWAPA MAFUNZO WAKUNGA 300!

                                         Baadhi ya wakunga wakiwa katika moja ya mkutano.
                  Wakunga wakiserebuka katika moja ya maadhimisho ya siku ya wakunga.
Wakunga takribani 300 nchini wanatarajia kupewa mafunzo kupitia mpango uliozinduliwa na Benki ya Barclays Nchini unaofahamika kama STEP AHEAD kwa lengo la kupunguza vifo vya kinamama vitokanavyo na uzazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mapango huo, Afisa Mkuu wa Mahusiano, Wa Bemki ya Barclays, KATI KERENGE, amesema lengo la mpango huo ni kusaidia utoaji wa huduma ya Afya kwa Mtoto mchanga na Mama Mjamzito ili kupunguza vifo vya kinamama vitokanavyo na uzazi nchini.
Aidha kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT, HAIKA MAWALLA, amesema mpaka sasa zaidi ya kinamama wajawazito 400 nchini hupoteza maisha kutokana na uzazi huku akibainisha kuwa mafunzo yatakayotolewa kwa wakunga ni pamoja na kuwafanyia oparesheni akinamama wenye matatizo ya fistula.

No comments:

Post a Comment