Thursday, June 9, 2011

WAKAZI JIJINI DSM WAIZUNGUMZIA BAJETI YA SERIKALI 2011/2012!

Waziri Mkulo na Bajeti hiyo Bungeni Mjini Dodoma jana.
Je Bajeti hii itamaliza kero kama hizi?
          Kwenye miundombinu, Je Bajeti hii itahakikisha fedha zilizotengwa zinatumika ipasavyo?
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wametoa maoni yao kuhusiana na Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 ambapo wameshangazwa na vipaumbele vya bajeti hiyo vilivyoanisha kuwa fedha za sekta ya Afya zimeongezwa kwa asilimia 0.3 wakati kukiwa na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo hususani katika maeneo ya vijijini.

Wakizungumza katika mahojiano maalum na kituo hiki wakazi hao wamesema bado suala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ni wa kusuasua hivyo serikali ilitakiwa kuelekeza nguvu zake katika kuboresha huduma za afya ili kupunguza vifo vinavyochangiwa na ukosefu wa dawa na matibabu.
Serikali imetangaza bajeti yake ya Shilingi trillion 13.5 iliyolenga kupunguza makali ya maisha wakati ikipandisha bei ya vinywaji baridi, bia na pombe kali huku ikitenga asilimia 14 yak bajeti yote kulipa deni la taifa.

No comments:

Post a Comment