Thursday, June 16, 2011

KAMPUNI YA STAR MEDIA LTD YAHITIMISHA KAMPENI YAKE YA STARTIMES NA WATOTO!

Kampuni ya Star Media Limited, imehitimisha kampeni yake ya Watoto na Startimes ambayo imedumu kwa takribani wiki mbili, ambapo katika kuunga mkono maadhimisho ya Mtoto wa Afrika Kampuni hiyo iliandaa shindano la kutafuta familia tatu bora zilizoshiriki katika kampeni hiyo.

Meneja masoko Msaidizi wa Kampuni hiyo, DAVIS MWIJAGE, amesema kampuni hiyo imeamua kutumia siku ya Mtoto wa Afrika kuwa kilele cha kampeni kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa familia tatu bora zilizoshiriki katika kampeni hiyo.
Ameongeza kuwa kampeni hiyo yenye kauli mbiu tutaijenga kesho iwapo tutawajengea watoto wetu mazingira mazuri, Afya na Elimu, ilihusisha baadhi ya mikoa nchini ikiwemo Mbeya, Tanga, Mwanza, Dodoma, Arusha na Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment