Monday, June 27, 2011

MNYIKA ASEMA MIRADI YA CDCF 2010/2011 KUANZA KUTEKELEZWA JIMBONI!

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, JOHN MNYIKA, amesema utekelezaji wa miradi iliyochangiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDCF) kwa mwaka wa fedha 2010/2011 awamu ya kwanza uko katika hatua za mwisho huku mchakato wa uteuzi wa miradi ya awamu ya pili umeanza.

MNYIKA amesema Miradi inayoendelea kutekelezwa kutokana na fedha za mfuko huo ni pamoja na ukarabati za Jengo la kutoa huduma ya afya kwa Wakina mama wajawazito na watoto katika Kata ya Kwembe ambao umetengewa shilingi milioni 27.3 pamoja na ujenzi wa kituo kidogo cha polisi Kata ya Ubungo Mtaa wa Msewe ambao unatarajia kugharimu shilingi milioni 6.
Ameongeza kuwa Jumla ya Fedha zilizotolewa na Mfuko huo katika awamu ya kwanza ni milioni 70 . 3 na kwamba Miradi mingine itakayo nufaika na Fedha hizo ni pamoja na Ujenzi wa Vyoo katika Shule ya Sekondari ya Hondogo Kata ya Kibamba Mtaa wa Kiluvya utakao gharimu milioni 22.
Katika Hatua nyingine Mbunge huyo amesema kuwa fedha za mfuko wa kuchochea maendeleo zilizotengwa kwa Jimbo la Ubungo katika mgawo wa awamu ya pili ni shilingi milioni 69 . 9 na kwamba fedha hizo zimetolewa kutoka Serikalini katika awamu mbili.

No comments:

Post a Comment