Thursday, June 16, 2011

SERIKALI KUFANYA UTAFITI JUU YA WATOTO WANAOISHI MITAANI NA KWENYE MAZINGIRA MAGUMU!

Serikali imeazimia kufanya utafiti ili kubaini idadi ya watoto waishio mitaani na katika mazingira magumu, ambapo sanjari na hatua hiyo ipo katika mpango wa kutenga bajeti maalum kwa ajili ya watoto hao.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi TUKAE NJIKU, amesema ipo haja ya kuanzishwa kwa mabaraza ya watoto kwenye shule mbalimbali nchini ambayo yatakuwa yakijadili na kuwasilisha matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo.
Kwa upande wake Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dawati la Jinsia na watoto, FELISTER MAUYA, ameitaka jamii kwa kushirikiana na Serikali pamoja na asasi binafsi kupiga vita ukatili dhidi ya watoto ambao unazidi kuongezeka hapa nchini kila siku.
Katika hatua nyingine watoto wamewaomba wazazi nchini kutoa kipaumbele kwa mtoto ikiwa ni pamoja na kumpa elimu ambayo ni miongoni mwa haki zake za msingi.

No comments:

Post a Comment