Friday, June 1, 2012

Nestle watoa zawadi kama sehemu kuu ya kusherekea siku ya maziwa Duniani

 Meneja wa Sayansi na Uthibiti wa Nestle Tanzania Marsha Yambi (kati) akikabizi zawadi kwa watoto wanaolelewa na kituo cha Chakuwama Orphanage zawadi ambazo ni moja ya Sehemu ya ushiriki wao katika kusheherekea siku ya Maziwa Duniani, Pamoja na watoto hao Pembeni ni mlezi wa kituo pamoja na maofisa wakuu wa Biashara Kutoka Kampuni ya Nestle Tanzania


 Bibi Mlezi wa Kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Bi. Khadija akifafanua jambo wa waandishi wa habari juu ya Changamoto anazozipata katika harakati za uendeshaji wa Vituo vya watoto yatima pamoja na Michango ya Taasisi mbalimbali kama Kampuni ya Nestle NIDO ilivyofanya kuwawezesha watoto kuwa na afya bora na kuhamasisha Unywaji wa Maziwa halisi ya Ng’ombe yaliokatika mifumo mbali mbali

 Mlezi wa kituo cha Kulea watoto yatima cha Tanzania Mitindo House na Mwanamitindo Maarufu Bi Khadija Mwanamboka akihojiwa na waandishi wa habari wakati akipokea zawadi kwa ajili ya kituo cha watoto yatima cha TMH ambapo Kampuni ya Nestle kupitia bidhaa ya NIDO imewawezesha vituo vitatu vya watuto yatima vya Dar es Salaam kusherehekea Siku ya Maziwa Dunia kwa kuwapa Maziwa ya NIDO na Bidhaa za MILO zenye thamani zaidi ya TSZ 5 Milioni.


Bidhaa za NIDO, CereVita, MILO kutoka Kampuni ya Nestle Tanzania zenye thamani ya TZS 5,548,800 Zilizogawiwa kwa vituo vyam kulea watoto yatima vya Umra, Chakuwama na Tanzania Mitindo house jijini dar es salaam zenye watoto takribani 200 wanaolelewa na vituo hivyo katika kuazimisha siku ya Maziwa Duniani ambayo hufanyika kila mwaka Juni 1st.

No comments:

Post a Comment